Jumatatu 25 Mei 2026 - 13:30
Kunyamaza mbele ya jinai ni sawa na kushirikiana na Marekani na Israe/ Wakati umefika wa kuchukua hatua, si kuwa watazamaji tu

Hawza/ Iqbal Korpinar, mwanaharakati wa Meli ya Samud nchini Uturuki, amesisitiza kwamba; kunyamaza mbele ya jinai zinazofanyika Ghaza na Minab ni kushirikiana na Marekani na Israel, amesema kuwa; wakati umefika wa kuacha kuwa watazamaji na kuelekea kwenye harakati za kijihadi, huku uma wa Kiislamu, uamke kiteknolojia na uchumi huru.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, katika kipindi cha televisheni “Mashahidi Watoto wa Minab, Sauti ya Madhlumiyyah ya Umma” kilichorushwa Jumamosi tarehe 2 Khordad 1405 (23 May 2026) kwa juhudi za Majma‘ Al-Alami Qadimun kupitia kituo cha Al-Kawthar, Iqbal Korpinar, mwanaharakati wa Meli ya Samud na mtetezi wa Palestina kutoka Uturuki, alitoa maoni yake kuhusu wajibu wa Umma wa Kiislamu mbele ya jinai zinazofanywa dhidi ya watoto wa Ghaza na Minab.

Akikosoa mtazamo wa uzembe wa baadhi ya Waislamu alisema: “Kwa miaka mingi tumeambiwa msisome simulizi za Kiyahudi, msifanye utafiti, salini tu na kaeni majumbani mkijishughulisha na mambo yenu, hii ndiyo ‘dawa ya kulevya ya kupooza fikra’ iliyosababisha ulimwengu wa Kiislamu kubaki nyuma katika nyanja ya teknolojia, lakini kwa bahati nzuri, maendeleo ya hivi karibuni katika sekta ya ulinzi ya Iran na Uturuki yamewatia hofu kubwa maadui kwa mara ya kwanza, kwa hiyo ni lazima tuamke.”

Iqbal Korpinar, akirejelea kuuawa kishahidi kwa maelfu ya watu kwa sababu tu ya kusema: «الله أكبر، أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمداً عبده ورسوله» na kutetea Msikiti wa Al-Aqsa, aliongeza: “Vipi tunaweza kuyafumbia macho maovu haya? Je, kwa kuomba dua na wakati mwingine kutuma kiasi kidogo cha fedha tunatuliza dhamiri zetu tu? Hili si jambo sahihi, ni lazima tuhamie kwenye ‘dua ya vitendo’.”

Akizungumzia hali ya kusikitisha ya watoto wa Palestina walioumia, alisisitiza: “Tunaona watoto ambao mikono na miguu yao imekatwa na kubaki na sehemu ya mwili pekee, maelfu ya watoto wamekatwa viungo na wanahitaji viungo bandia, lakini hata kama tutawapatia viungo hivyo, ni nani atakayewarudishia mama zao, baba zao na kumbukumbu zao? Je, magofu ya ndoto zao yanaweza kujengwa upya? Jeraha hili la kina la kisaikolojia litaponywaje?”

Mwanaharakati huyo wa Palestina aliuliza swali la msingi: “Kwa nini tunanyamaza mbele ya dhulma yote hii? Watu wote wanaonyamaza mbele ya jinai hizi huku wakiwa na uwezo wa kuzungumza, kwa kiwango cha chini wanawajibika kwa jinai hizi sawa na Israel na Marekani, ninaamini kwamba tatizo kubwa zaidi la ulimwengu wa Kiislamu si ‘kukosa ufahamu’, bali ni kukosekana kwa ‘ufahamu wa Kiislamu’.”

Akirejelea kujitolea kwa Maswahaba wa Mtume (saww), alisema: “Je, Mtume Mtukufu (saww) na Maswahaba wake hawakuueneza Uislamu kwa kutoa maisha na mali zao? Leo waandishi wa habari wa Ghaza wanatukumbusha maisha ya Maswahaba, hata katika shahada yao wanafundisha ubinadamu, watu katika mitaa ya Uingereza, Hispania, Marekani na nchi nyingi nyingine wameamka, na hakuna anayoweza tena kuwadanganya.”

Iqbal Korpinar alieleza uzoefu wake binafsi na kusema: “Mimi mwenyewe ni miongoni mwa wale walioanza safari ya kwenda Ghaza; kutoka Tunisia hadi Cyprus, lakini niliporudi Uturuki, nilikumbana na mashambulizi makubwa sana katika mitandao ya kijamii, yaani wimbi la matusi, vitisho na tuhuma kutoka kwa watu wengi, kwa sababu Wazayuni wamepenya miongoni mwetu, baadhi yao walikuja Uturuki miaka mingi iliyopita na kubadilisha majina yao ya familia pamoja na dini zao, kwa muda ambao mitandao ya kijamii iko mikononi mwao, si rahisi kwetu kupambana na operesheni za vita vya kisaikolojia.”

Alizitaka nchi za Kiislamu kuanzisha mitandao yao ya kijamii iliyo huru na akaendelea kusema: “WhatsApp, Instagram na YouTube zote ziko mikononi mwa Wazayuni. WhatsApp hivi karibuni ilitoa msaada mkubwa wa kifedha kwa Israel, kuanzia viwanda vya chakula, vipodozi, teknolojia, tiba na kila kitu unachoweza kufikiria, wamepenya katika nyanja zote, lakini je, tunauona uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwa mdogo mbele ya uwezo wao? Mwenyezi Mungu amesema:

وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

‘Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wanaopanga mipango.’”

Mwanaharakati huyo wa Palestina, akirejelea aya ya Qur’ani Tukufu, alisema: “Mwenyezi Mungu hamruhusu Muumini kukaa kimya mbele ya dhulma inayomfika ndugu yake wa dini, hatutawahi kupuuza jihadi, Uislamu haujatuahidi Pepo duniani; bali Uislamu unatufundisha kwamba dunia ni ya kupita, kifo hakiko mbali nasi; ninaweza kufa sasa hivi ndani ya nyumba yangu, lakini sitaki kifo cha namna hiyo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, nataka kuwa shahidi.”

Mwisho, akirejelea kulengwa kwa watoto na wanawake na maadui, alisema: “Kwa nini wanawalenga watoto? Ili kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu na kupunguza idadi yao, wanataka kuwaua wanawake na watoto ili Waislamu wasiweze kuzaana na hatimaye wajisalimishe, hapana, hilo halitatokea, Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru Yake, lakini anatutaka tuwe na ghera na juhudi.

Hawa watu hawaui Waislamu kwa silaha na mabomu pekee, bali pia kupitia vyakula, nepi za watoto, karatasi za chooni, dawa za kuzuia uzazi na virutubisho vya lishe, huku wakichukua fedha zetu pia, kila nchi ya Kiislamu inapaswa kuzalisha bidhaa zake za ndani na kwa kadiri iwezekanavyo kuepuka kutumia bidhaa zao.

Je, sisi hatuna akili? Je, Mwenyezi Mungu hasemi mara nyingi ndani ya Qur’ani:

أَفَلَا تَعْقِلُونَ

‘Je, hamtumii akili zenu?’

Sisi pia tunaweza kung’ara na kuzalisha kwa kutegemea akili na vipaji vyetu wenyewe, kama walivyofanya Ibn Sina na Al-Khwarizmi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha